Tundu Lissu asimama....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu

HALI ya kiafya ya mwanasheria mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu inaendelea kuimarika na sasa ameanza kusimama kwa mguu mmoja akitumia msaada wa wahudumu wa hospitali anayotibiwa nchini Kenya.

Lissu ambae pia ni mbunge yupo katika Hospital ya Nairobi nchini Kenya anakoendelea na matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwezi Septemba, 2017

Tundu Lissu katikati akiwa amesimama akisaidiwa na wahudumu wa hospitali

Katika taarifa aliyoandika leo, Tundu Lissu anasema:

Dear family na wapendwa wote.
Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema 'nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.'

Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa 'Mababa Cheza' wangu.

Hatua inayofuata ni magongo, kesho  nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu accordingly.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search