Samia Suluhu: Ukimwi unawaathiri zaidi wasichana, awaonya 'mashugadadi'...soma habari kamili na matukio360..#share
Salha Mohamed
TAKWIMU zinaeleza kuwapo kwa ongezeko la takribani watu 9000 walioambukizwa virusi vya ukimwi nchini kutoka mwaka 2013 watu 72,000 hadi 81,000 mwaka 2017. Waathirika zaidi ni wasichana wenye umri kati ya miaka 15-24.
Kufuatia hali hiyo makamu wa rais Samia Suluhu amewaonya wanaume 'mashugadadi' kuacha kujihusisha na vitendo vya ngono na wasichana wadogo na kwamba watulizane na wavumilie kuwa na wake zao.
Kufuatia hali hiyo makamu wa rais Samia Suluhu amewaonya wanaume 'mashugadadi' kuacha kujihusisha na vitendo vya ngono na wasichana wadogo na kwamba watulizane na wavumilie kuwa na wake zao.
Makamu wa rais Samia Suluhu akihutubia hii leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kilele cha siku ya ukimwi Duniani
Takwimu hizo ni kati ya watanzania milioni 1.4 wanaoishi na virusi vya ukimwi huku waathirika zaidi wakiwa ni wasichana wenye umri kati ya miaka 15-24.
Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua takwimu mpya za viashiria na ushamiri wa ukimwi Tanzania
kwa mwaka 2016/2017 ikiwa ni kilele cha maandhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.
“Takwimu zinaonesha baadhi ya mikoa inamaambukizi
zaidi ya kiwango cha taifa cha asilimia 5 ambapo Mkoa wa Njombe una asilimia
11.4, Iringa asilimia 11.3, Mbeya asilimia 9.3,Mwanza asilimia 7.2, Kagera asilimia
6.5, Shinyanga asilimia 5.9 na Katavi kwa asilimia 5.9,”amesema.
Ameongeza mikoa mingine ni Songwe kwa asilimia 5.9,
Rukwa asilimia 6.2, Dar es Salaam kwa asilimia 6.9, Ruvuma asilimia 5.6 na
Pwani kwa asilimia 5.5.
Amesema bado kuna changamoto ya ulevi wa kupindukia
na watu kufanya ngono zembe, kuwa na wapenzi wengi hivyo jamii inapaswa kuacha
tabia hizo kwani serikali haiwezi kuyaingilia ni masuala binafsi.
Amefafanua kuwa mila hatarishi zimekuwa zikichangia
maambukizi ya virusi vya ukimwi kama ngono na ndoa za utotoni ,kurithi
wajane kuacha.
Samia amewataka viongozi wa dini kuwaasa wanaume na
vijana hasa wakike kutojiingiza kwenye janga hilo.
“Wanaume wote wa Tanzania mmekuwa na tamaa, muwe na
maadili mnahisi wazee wenzenu wamechuja mnaenda kwa watoto mjue kuwa hili ni
taifa letu …huu ni uuaji waacheni watoto wa kike waendelee na maisha,”amesema.



No comments:
Post a Comment