Wapinzani Zimbabwe wamshutumu Mnangagwa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mashirika ya Kimataifa
UPINZANI nchini Zimbabwe umelaumu kitendo cha rais mpya wa nchi
hiyo, Emmerson Mnangagwa kuteua maofisa wakuu wa jeshi kuwa mawaziri katika
baraza jipya alilolitangaza.
Rais wa Zimbabwe,Emmerson Mnangagwa.
Umedai mabadiliko hayo ni
kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia kutokana na kwamba vikosi vya
usalama vilikuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe ambavyo hadi
sasa vinaendelea kuthibiti taifa hilo.
Kiongozi wa upinzani, Tendai Biti amesema fungate
iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.
Katika baraza hilo Mnangagwa amemteua
ofisa mkuu wa jeshi kuwa n awadhifu mkuu katika serikali yake.
Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo ambaye ndie jenerali aliyetangaza
katika runinga ya taifa hilo kuwa jeshi limechukua
udhibiti na kumzuia nyumbani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mubage.
Mkuu wa jeshi la angani, Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha
na kilimo.
Imedaiwa kuwa umoja ulioonekana katika siku za karibuni huenda ukabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Rais Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu
kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka 39.




No comments:
Post a Comment