Serikali isimamie majukumu yake ipasavyo...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora (THBUB) Bahame Nyanduga
Pia imeishauri serikali kuhakikisha inasimamia majukumu yake
ili kukomesha vitendo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo hufanyika
kila Desemba 10 iliyoandaliwa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) mwenyekiti
wa THBuB Bahame Nyanduga, ametaja vitendo hivyo kuwa ni uminywaji wa uhuru wa
kujieleza, siasa, watu kupigwa na kuumizwa, utekwaji na kupotea.
“Kwakeli tume inekemea jambo hili na Tunaishauri serikali
kama ilivyo wajibu wake kwamba isimamie majukumu yake kuhakikisha vitendo hivi
vinakomeshwa ili Tanzania isifikie mahali ikaonekana kama ni nchi ambayo
haiheshimu haki za binadamu,” amesema.
“Kwa sababu hadi sasa sifa hiyo bado tunayo lakini naona
taratibu sifa hiyo inaanza kuporomkoa,” ameongeza.
Nyanduga amesema tume haifurahishwi na vitendo hivyo na
kwamba wamekuwa wakipokea malalamiko na kuyafanyia uchunguzi dhidi ya matukio
hayo na kuyatolea matamko pamoja na kuishauri serikali ili ichukue hatua.
“Chamsingi naweza kusema ni kwamba kazi kubwa ya tume ni
kuhakisha ina simamia misingi mbalimbali ya haki za binadamu na utawala bora
ili tujenge jamii ineyoheshza binadamu imu haki,” amesema.
Amevitaka vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi haraka dhidi
ya vitendo hivyo ili kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika wa vitendo
hivyo , lakini pia mahakama zifanye kazi yake kwa uadilifu.
Amesema kulinda na kuheshimu haki za binadamu ni wajibu wa
kila mtu na kueleza kuwa serikali
inawajibu mkubwa zaidi wa kuzilinda kwani ni mwanachama wa mikataba mingi ya
kimataifa ya kuhusiana na masuala ya haki za binadamu.



No comments:
Post a Comment