Serikali yaitaka taasisi elimu ya watu wazima kuandaa wataalam..soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu,Dar es salaam
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wiliam Ole Nasha ameiagiza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kurejea jukumu lake la msingi la kuwaandaa wataalamu katika fani za Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii.
Ametoa agizo hilo katika mahafali ya 53 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesaba (KKK) kwa vijana na watu wazima.
"Eneo la Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi bado linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa Vituo na walimu wenye ujuzi stahiki katika ngazi ya ElimuMsingi" amesisitiza Naibu Waziri.
Ole Nasha amesema Wizara tayari ilishatoa Mwongozo wa shule za Msingi na Sekondari kutumika kama vituo vya kutolea Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rsami, wakati utaratibu wa kuvitumia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) unaandaliwa ili kuwezesha upatiknaji wake.
Naibu waziri amesema kiasi cha silingi Bilioni 1.8 kimetengwa kwa ajili ya mafunzo maalum kwa walimu 1,545 kwa mwaka 2017/18.
Naibu Waziri amesema serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutekeleza Mipango mbalimbali ambayo inawawezesha vijana na watu wazima waliokosa fursa katika Mfumo Rasmi wa Elimu kujiendeleza kielimu na kumudu changamoto za maisha, ambapo alitaja mipango hiyo kuwa ni Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) na Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA).
Aidha, Ole Nasha amewataka wahitimu kwenda kufanya kazi kwa ueledi zaidi ili kusaidia jitihada za Serikali za kupambana na adui ujinga na hivyo kulifikisha taifa katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Naye Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Fidelice Mafumiko amesema taasisi I naendelea kuongeza fursa zaidi katika utoaji elimu kwa kupitia programu za mafunzo kwa kutumia njia ya ujifunzaji huria na masafa kwa ngazi ya Stashahada.
Dk Mafuniko amasema hadi sasa Taasisi imeongeza vituo vya mafunzo vya Elimu ya Watu Wazima kutoka vituo 13 hadi kufikia 21 katika mikoa13.

No comments:
Post a Comment