Serikali yatakiwa kuongeza nguvu elimu magonjwa yasiyoambukiza..soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed,Dar es salaam
SERIKALI imeombwa kutoa mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza kwa walimu ili kujua namna ya kuishi na kuwasaidia wanafunzi wenye magonjwa hayo pindi wawapo shuleni.
Wanafunzi, walimu na baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ilala wakifanya mazoezi

Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza
Dar es Salaam, Dk. Digna Riwa amesema wakati wa ufunguzi wa mchakamchaka kwa wanafunzi wa shule za msingi kuwa serikali iongeze vifaa tiba pamoja na wanafunzi kukimbia mchakamchaka kabla ya kuingia darasani.
"Tunaona kwamba kuna watoto wengi wanapoteza maisha wakiwa shuleni kwasababu mwalimu haelewi afanye nini, "amesema.
Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya afya (2012) asilimia 27 ya vifo hapa nchini husababishwa na magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza(CCP),Dk. Frank Manace amesema athari za magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari, shinikizo la damu, asthma, na saratani, imekuwa
chanzo kikubwa cha maumivi ya kimwili, kiakili na kiroho kwa familia nyingi za Kitanzania.
"Miezi sita iliyopita tulikuwa hapa... na tuliweka kambi ya upimaji afya ya wiki nzima ambapo tulipima watoto na vijana magonjwa ya moyo, seli mundu (sickle cell disease) afya ya akili, afya ya kinywa na meno, afya ya pua koo na masikio.
Amesema katika kambi hiyo walibaini kuwa katika kila watoto 100, watoto 7 wanamatatizo ya moyo ambapo kati ya watoto 10 watoto 4 wana shida ya macho na kati ya watoto 10, watoto 6 wana matatizo ya meno.
Amesema walistuka kuona mtoto wa darasa la tano ambaye alikuwa hajui kusoma ambapo walibaini hakuwa na uwezo wa kusikia kutokana na nta ambayo imeganda masikioni.
"Tulikutana na mtoto mwenye kisukari tangu uzaliwa ila mpaka alipofikia miaka mitano wazazi wala walimu hawakuweza kufahamu.
"Wapo watoto waliowekwa katika kundi la watoto wazito au ( Slow lerners) na tuligundua kumbe baadhi yao ni kwa sababu ya shida ya uoni/macho,"amesema na kuongeza kuwa
"Mtoto mwenye matatizo ya moyo, sickle cell, au pumu (asthma) ukimwabia akimbie mchakamchaka na watoto wengine atakuwa wa mwisho kuanza, atahitaji kupumzika mara nyingi njiani, hataweza kumaliza kama ambavyo wenzake wangefanya,"amesema.
Amesema magonjwa hayo huweza kusababisha vifo vya ghafla pindi mtoto mwenye pumu asipopata huduma ya haraka, sahihi, na wakati huweza upoteza maisha ndani ya dakika chache.
Dk. Manace amesema kufahamu mtoto mwenye pumu ni muhimu kuliko kuwa na wodi ya kumlaza anapo shikwa na pumu.

About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment