Serikali yazionya taasisi za kidini...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi kitengo cha ofisi ya msajili wa jumuia za kidini imezionya taasisi za dini kufuata katiba zao na kwamba kujihusisha na siasa ni kinyume  cha sheria.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi

Taarifa iliyotolewa leo na katibu  mkuu  wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) inasema: "Baadhi ya Jumuia  zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili. 

"Mathalani hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa Jumuia kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao kwani hakuna Jumuiya yoyote iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Jumuiya ili kufanya kazi za siasa.

"Tabia hii ni kwenda kinyume na malengo na ni ukiukaji Kanuni ya 7 ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya Sheria ya Jumuiya, inayotamka kwamba Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya malengo yake bila ya kibali cha Msajili."


Taarifa hiyo inaeleza kuwa miongoni mwa masharti yanayopaswa kuzingatiwa na Jumuiya hizo ni pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya Katiba zao ambazo pamoja na mambo mengine  hueleza malengo ya Jumuiya husika.

Hata hivyo, Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote zinazofanya kazi kinyume na malengo yaliyoainishwa katika Katiba zao zilizosajiliwa kuacha kufanya hivyo mara moja. 

Inaeleza Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuia zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search