Zanzibar Heroes yapokelewa shughuli zasimama 'Zenji'...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KIKOSI cha timu ya Taifa ya
Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kimerejea visiwani leo na kupokelewa kwa shangwe
kubwa na mashabiki na wananchi wa Zanzibar.
Kikosi cha Zanzibar Heroes
Kikosi hicho ambacho
kimepata nafasi ya pili katika
mashindano ya Chalenji nchini Kenya kiliwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa kwa ndege ya kukodi ya Tropical majira ya saa 6:15 za mchana.
Kikosi hicho kilichoongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na
Michezo Rashid Ali Juma, kilipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Ayoub Mohammed Mahmoud.
Katika mapokezi hayo
wananchi na viongozi mbali mbali walijitokeza kuja kuwalaki kwa kuimba
nyimbo mbali mbali ikiwemo wimbo wa Sisi Sote ambao huimbwa mara nyingi wakati
wa sherehe za Mapinduzi.
Msafara wa wachezaji hao
ulianza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa na kupitia Kiembe Samaki,
Mwanakwerekwe, Amani na kumalizikia katika Mnara wa Kumbukumbu uliopo Kisonge
mjini Unguja.
Wakati wachezaji hao
wakipita katika barabara hiyo walishangiliwa kwa shangwe na wananchi waliokaa
pembezoni mwa njia hizo huku shughuli nyingi za kijamii zikisita.
Timu ya Taifa ya Zanzibar
ilikuwa nchini Kenya kushiriki michuano ya Chalenj ilifikia hatua ya fainali na
kufanikiwa kupata nafasi ya pili kufatia kufungwa na wenyeji Kenya kwa
penant 3-2 .
Timu hizo ziliweza kupigiana mikwaju ya penati baada
ya kumaliza dakika 120 wakiwa sare ya mabao 2-2 hatua ambayo ilifikia hilo kutokana
na kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya kufungana bao 1-1.
No comments:
Post a Comment