Taasisi ya JK yawafanyia operesheni ya moyo watu 16...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) ikishirikiana na taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini
Australia wamefanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa
16 wenye matatizo ya Moyo, kati ya hao watoto ni tisa
Madaktari wakifanya upasuaji
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo
vya habari leo na kitengo cha Uhusiano na Masoko JKCI, upasuaji huo umefanyika katika
kambi maalum ya matibabu ya Moyo iliyoanza Novemba 25, 2017 na kumalizika leo
Desemba 01, 2017.
Wagonjwa watu wazima wamewafanyia
upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG Coronary Artery
Bypass Grafting) na kubadilisha milango ya moyo miwili hadi mitatu iliyokuwa
imeziba au haifungi vizuri.
Kwa upande wa watoto
wamefanya upasuaji na vipimo kwa watoto ambao vyumba vyao vya moyo
havijakamilika na hivyo damu kwenda kwa wingi kwenye mapafu. Kuwafanyia watoto
vipimo tukiwa tumefungua vifua inasaidia kufahamu aina ya upasuaji
tunaotakiwa kuufanya.
Upasuaji uliowafanywa
kwa watoto ni wa awali ili kuutayarisha moyo kwa ajili ya upasuaji
mwingine ujao.
Watoto waliofanyiwa upasuaji
katika kambi hiyo ni wenye uzito wa kuanzia kilo nne hadi 12 ambao umri
wao ni miezi minne hadi miaka minne.
Kwa mara ya kwanza wameweza
kufanya upasuaji kwa mtoto ambaye moyo wake ulikuwa upande wa kulia na
vyumba vyote vya moyo vinafanana wakati vinatakiwa kuwa tofauti .
Katika upasuaji huo wameweza
kulinda mapafu yalikuwa yanapokea damu kwa wingi kutoka kwenye mishipa ya
moyo. Mtoto huyu pia tumeweza kumuwekea kifaa ambacho kitamsaidia moyo wake
kufanya kazi vizuri (Pace Maker).
JKci imewashukuru OHI kwa kuona umuhimu wa kushirikiana nao
kutoa matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo paoja na kuwapatia mafunzo ambayo
yamewasaidia kuongeza ufanisi wa kazi.
Kabla ya kuanza kambi hiyo kulikuwa
na mafunzo kwa wauguzi wa JKCI ambao walifundishwa jinsi ya kuwahudumia
wagonjwa waliopo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).
Wananchi wameombwa kuendela
kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji
kuongezewa damu wakati wanapatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment