TTCF: Sheria kudhibiti tumbaku itungwe....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed, Dar es salaam
TANZANIA ndio nchi pekee Afrika Mashariki ambayo haina
sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Pia kila mwaka takribani watu milioni 7 Duniani
hufariki kutokana na matunizi ya tumbaku na
watu 700,000 wakivutishwa moshi wa tumbaku.
Mkurugenzi mtendaji wa chama cha kudhibiti Tumbaku Tanzania(TTCF) lutgard Kagaruki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kushoto ni mwandishi wa habari za uchunguzi, David Rwenyagira na Mwansheria wa kituo cha Sheria na haki za binadamu(LHRC), Tito Magoti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku
Tanzania(TTCF)), Lutgard Kagaruki ameyasema hayo jijini Dar es Salaam
“Tumeshtushwa
na tamko la Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba kuhusu mkataba wa kimataifa wa
kudhibiti tumbaku wa shirika la afya
Duniani na ameubeza akidai unazuia kilimo cha tumbaku.’’ amesema Kagaruki na
kuongeza “Nchi ilisaini mkataba huu mwaka 2007 ni wajibu kuutekeleza.”
Amesema utafiti unaonesha mwaka 2013 asilimia 14 ya
watanzania ni wavutaji huku wanaume wakiwa na asilimia 2.9
Amesema
asilimia 17.5 ya wasiovuta sigara huvutishwa moshi wa tumbaku majumbani na
asilimia 24.9 huvutishwa moshi huo mahala
pa kazi huku matokeo ya Global youth tobacco survey (2008) yakionesha asilimia
9.7 vijana ni wavutaji.
Amesema utafiti wa awali (2009) wa taasisi ya saratani
ya ocean road unaonesha asilimia 32 ya saratani katika taasisi hiyo
zilihusishwa na matumizi ya tumbaku zikiligharimu taifa dola za marekani
milioni 40 kwa matibabu.
"Pale Hospitali ya taifa Muhimbili, utafiti ulibaini serikali ilikuwa inatumia
dola za kimarekani milioni 186 kutibu magonjwa ya moyo yaliyohusishwa natumizi
ya tumbaku, "amesema.
Amesema kilimo cha tumbaku kinawaumiza wakulima kutokana na kemikali ya
nikotini ambayo hupenya kwenye ngozi na hewa wanayovuta.
Amesema kilimo cha tumbaku bado kinaendelea kuongezeka
kwa kasi na kwamba kinanufaisha kampuni
za tumbaku na si wakulima.
Mwanasheria wa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Tito Magoti amesema mkataba huo haujalenga
kuzuia, umelenga matumizi sahihi ya tumbaku.
No comments:
Post a Comment