Mohamed Salah mshindi tuzo ya BBC 2017...soma habari kamili na matukio360..#share
Na masharika ya kimataifa
MOHAMED Salah wa Misri amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo
ya BBC kwa Mwanasoka bora wa Afrika Mwaka 2017.
Mohamed Salah
Nyota huyu wa Liverpool
alipata kura nyingi zaidi ya Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Naby Keïta wa
Guinea, Sadio Mané wa Senegal na mchezaji wa Nigeria Victor Moses.
"Nimefurahi sana kupata
tuzo hii," mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliiambia BBC Sport.
"Huwa ni hisia ya kipekee unaposhinda kitu.
Unahisi ulikuwa na mwaka mzuri sana. Kwa hivyo nina furaha sana. Ningependa
kushinda tena mwaka ujao!"
Salah, aliyefunga mabao mengi zaidi ligi kuu England,
akiwa na mabao 13, amekuwa na mwaka wenye mafanikio.
Mapema 2017 alikuwa nyota wa Misri walipochukua nafasi
ya pili katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Baadaye mwakani, mshambuliaji huyu aliye na kasi
alichangia katika magoli yote yaliyowasaidia Mafarao kufuzu kushiriki michuano
ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990 - aliwasaidia wenzake kufunga
mabao mawili, naye akafunga mabao matano, moja ikiwa penalti kati yao na Congo
iliyowawezesha kufuzu kwa fainali hizo za Urusi.
"Ninataka kuwa
mwanakandanda bora zaidi wa Misri kwa hivyo mimi hutia bidii," anasema
kijana huyu ambaye amekuwa raia wa tatu wa Misri kupata tuzo hii tangu 2008.
"Mimi hufuata njia
yangu na ninataka watu wote Misri kufuata njia yangu"
No comments:
Post a Comment