Ushahidi kesi ya Wema Sepetu kuanza kutolewa...soma habari kamili na matukio360..#share
Abdulrahim Sadiki,Dar es Salaam.
USHAHIDI wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili msanii wa filamu, Wema Sepetu utaanza kusikilizwa Januari 10,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wema Sepetu
Leo kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Wakili
wa Serikali, Costantine Kakula ameeleza wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi
na wana mashahidi wawili.
Kutokana na maelezo hayo, Wakili wa utetezi, Devotha
Kianga kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe
nyingine.
Kwa kuwa wakili Kibatala ambaye anawatetea,Wema na wenzake wawili,
hakuwapo katika Mahakama ya Kisutu alikuwapo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi
kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba ameiahirisha
kesi hiyo hadi Januari 10,2018.
Wengine wanaokabiliwa katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni
Angelina Msigwa na Matrida Seleman
Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa
na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa
kuwa Februari 4,2017 katika
Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio
washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye
uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi,
2017 katika eneo lisilojulikana jijini
Dar es Salaam, alitumia dawa za
kulevya aina ya Bangi.
Wema ni miongoni mwa watu
waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha
na dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Februari 3,
2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.
No comments:
Post a Comment