Magufuli apiga marufuku kucheza ukiwa mtupu...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa taifa wa CCM, Dk John Magufuli amekemea vikali watu wanaocheza muziki wakiwa watupu ili kulinda maadili ya taifa.

Pia amewataka wadau wote kulinda maadili ya watanzania na kwamba uchezaji muziki ukiwa mtupu ni kinyume na maadili ya watanzania.
Mwenyekiti wa CCM taifa, John Magufuli

Ametoa agizo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa jumuiya ya wazazi wa CCM. Katika mkutano huo watachaguliwa viongozi wapya wa jumuiya hiyo

‘’Kila kitu kinamahala pake hivyo haiwezekani watu wacheze wakiwa uchi katika muziki. Hili likemewe na halipaswi kuchekelewa,’’ amesema Magufuli

Pia ameitaka jumuiya hiyo kuikemea serikali kama itakwenda kinyume na maadili.

‘’Pia wajibu wenu ni kuikemea Serikali ikienda kinyume na maadili na pia mdhibiti na mkishindwa basi mkemee uvunjifu wa maadili,’’ amesema.

Pamoja na mambo mengine ameitaka jumuiya hiyo kuipa serikali shule inazozimiliki ili iziendeleze kwa maslahi ya umma.


Amesema serikali ipo tayari kuchukua angalau shule kumi kati ya 54 zinazomilikiwa na jumuiya hiyo na kwamba serikali itawalipa fedha za ununuzi wa shule hiyo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search