UTAFITI: Wanaume wanamfumo dhaifu kuliko wanawake ...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
UTAFITI mpya unaashiria kwamba ni kweli wanaume hutatizwa na mafua zaidi kuliko wanawake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa dhana kwamba huwa kuna mafua ya wanaume.

Watafiti nchini Canada wanasema wamepata ushahidi kwamba wanaume hutatizwa zaidi na mafua ya kawaida na si kwamba huwa wanajifanya kwamba wamezidiwa.
Mtafiti mkuu Dk Kyle Sue amesema wanaume huenda wana mfumo dhaifu kidogo wa kinga mwilini dhidi ya virusi vinavyosababisha mafua wakilinganishwa na wanawake.
Hilo huenda  huchangia kuelemewa  na dalili za mafua kuliko wanawake.
Dk Sue anadokeza kwamba wakati umefika pengine kwa wanaume "kutengewa au kutengenezewa maeneo mahsusi, yaliyo na televisheni na viti vizuri, ambapo wanaweza kuuguza mafua yao hadi wapate nafuu bila usumbufu."
Matokeo ya utafiti huo huenda yakafurahiwa sana na wanaume wengi wanaotatizwa na mafua ambao wamehisi kwa muda mrefu kwamba hakujakuwa na watu wa kuwaelewa.
Lakini huenda yasiwafurahishe wanasayansi wengi  ambao  bado wana shaka kuhusu iwapo ni kweli kuna 'mafua ya wanaume' au huwa tu katika fikira za wanaume.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search