Marekani yaibembeleza Korea Kaskazini...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
WAZIRI wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema nchi yake ipo tayari kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote.
Rex Tillerson, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Amesema lengo kuu la mazungumzo hayo ni kuweka mambo sawa na kufikia makubaliano yenye amani bila kuwepo kwa vita.
Tillerson ameonya kuwa mazungumzo hayo yatafanyika tu iwapo Korea Kaskazini itasitisha majaribio yake ya makombora ya nyuklia.
Ameitaka Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo.
"Tupo tayari kwa mazungumzo muda wowote na Korea Kaskazini,tena mazungumzo yasiyo na masharti.Hebu tukutane.Hatuwezi kuzungumzia namna mpangilio wa mazungumzo hayo,utakavyo kuwa kama ni meza ya duara ama la,Lakini je tunaweza kukaa chini uso kwa uso tujadili jambo hili?na kisha kuanza kuweka namna ya kufikia maridhiano. "
Rex Tillerson amekuwa akifanya kila linalowezekana kusaka suluhu ya mzozo wa taifa lake na Korea Kaskazini kwa njia ya majadiliano na si vita.
No comments:
Post a Comment