Waziri awaonya wajumbe wapya bodi za utalii...soma habari na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam 
NAIBU waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema hatasita kuwatumbua watendaji wa vyombo vinavyosimamia biashara ya utalii nchini endapo hawatafikisha idadi ya watalii milioni mbili ifikapo 2020.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet  Hasunga
Hasunga ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua vyombo vya kusimamia biashara za utalii nchini.
"Tukishindwa kufikia lengo hili kabla sisi hatujatumbuliwa, tutawatumbua kwanza ninyi kwani tumewapa dhamana mtusaidie kama hatufikii malengo maana yake kazi haijaenda sawasawa, "amesema.
Amesema vyombo hivyo ni bodi ya Leseni za biashara ya utalii, Kamati ya Ushauri na Mamlaka ya rufaa.
Amesema sekta hiyo ni mtambuka hivyo kila mtu anawajibu wa kulinda rasilimali ,hifadhi za nchi ili kuongeza mapato ya nchi na wageni kujifunza tamaduni za nchi.
"Utalii ni miongoni mwa sekta katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu,katika ajira za moja kwa moja na hata kuchangia pato la taifa na fedha za kigeni, "amesema. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Aloyce Nzuki amesema vyombo hivyo vinatoa mchango katika kusimamia na kuendeleza sekta ya utalii kwa kutimiza malengo yake kwa mujibu wa sheria ya utalii Na. 29,2008 na kanuni zake za mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ,Profesa Wineaster Anderson amesema sekta ya utalii inaongeza asilimia 18 ya pato la taifa huku akiahidi kufanya kazi kama sheria inavyosema.
 
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:
Post a Comment