Wakamatwa wakiwa na sare za JWTZ...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia
Lainon Fratenus Lwegasira (20) mkazi wa Mahenge mkoani Morogoro na Noel
Cleophace Wagesa (30) mkazi wa kigogo jijini Dar es Salaam kwa kosa la kukutwa
wakiwa wamevaa sare za jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Katikati ni Lainon Fratenus Lwegasira (20), mmoja kati ya wawili waliokuwa na sare za JWTZ, akihojiwa na SACP Lazaro Mambosasa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi
Kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa, amesema watuhumiwa waliwakamata Desemba 15,
2017 majira ya saa 6:00 usiku eneo la Lugalo Kawe.
“Polisi wakiwa katika doria walifanikiwa kuwakamata vijana
hao wakiwa wamevaa sare za JWTZ na kisu kimoja huku wakitumia gari no. T 306
CRU Toyota Carina rangi ya fedha,” amesema SACP Mambosasa.
Amesema kuwa watuhumiwa hao wanasadikiwa kujihusisha na
matukio mbalimbali ya uporaji jijini humo, kabla ya ukamatwa kwao kulipatikana
taarifa kuwa kuna watu wanne kati yao mmoja amevaa sare za jeshi na wanafanya
uporaji ndipo askari walipofuatilia na kuwakamata.
Amesema watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao
mzima na matukio yote waliyowahi kuyafanya. Na baada ya upelelezi kukamilika
watuhumiwa watapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi nyingine za kisheria.
Mmoja wa watuhumiwa Lwegasira akihojiwa na kamanda Mambosasa alipozipata
sare hizo, na alikuwa akizitumiaje, amedai kuwa alipewa na rafiki yake
aliyemtaja kwa jina la Frank.
Amesema alikuwa akizitumia katika kusafirishia mizigo
hususani televisheni kutoka Zanzibar na kuzipeleka Tabata na amefafanua kwamba
alikuwa akizivaa pindi wanaposafirisha mzigo kwenye gari ili wasikamatwe.




No comments:
Post a Comment