Afanyiwa upasuaji wa tumbo mara kumi hapati haja kubwa, anatapika....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed,Dar es Salaam
MSICHANA Mariam Mwema(16),anayesumbuliwa na utumbo kujikunja 'Intestinal Obstruction ' anahitaji milioni 44 kwa ajili ya matibabu Apollo nchini India.
Mkurugenzi wa Masoko wa Data Vision International, Teddy Qirtu (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) uzinduzi wa kampeni ya kusaidia matibabu ya Mariam Mwema anayetarajia kufanyiwa upasuaji hospitali ya Apollo nchini India.
Mariam anayesoma kidato cha nne shule ya sekondari Kawe-Ukwamani utumbo wake umejikunja na kusababisha kufunga na kuzuia chakula kupita jambo linalosababisha kutapika kila anachokula na kutopata haja kubwa.
Kutokana na tatizo hilo, mariam amefanyiwa upasuaji wa tumbo mara kumi katika hospitali ya taifa Muhimbili(MNH),bila mafanikio.
Mkurugenzi wa Masoko wa Data Vision Internacional, Teddy Qirtu amesema leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua kampeni ya 'Tuko pamoja' kuwa Mariam ameshindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kutokana na tatizo alilonalo.
"Ameanza kusumbuliwa na ugonjwa huu tangu 2009 na ndipo alipofanyiwa upasuaji wa kwanza,hadi mwaka huu amefanyiwa upasuaji wa tumbo mara kumi...madaktari wetu wa Muhimbili wameshauri akatibiwe nchini India," amesema.
Amefafanua kuwa "Kwa mujibu wa madaktari wa Apollo nchini India, yatagharimu dola za marekani 20,000 ambapo dola 10,000 kwaajili ya upasuaji na dola 10,000 kwa ajili ya huduma zingine za kitabibu, "amesema.
Amesema kutokana na hali ya kiuchumi wazazi wake wameshindwa kugharamia matibabu hayo na kuamua kupaza sauti kwa umma na kutafuta utatuzi.
"Kupitia kampeni ya tuko pamoja inalenga kumulika matatizo ya jamii,kushirikiana na kuyatatua,tuliamua kumilika tatizo la mariam, "amesema.
Amesema wanaendelea kupokea michango ya fedha kwa wadau kwa njia ya simu za mkononi ambapo mchangiaji anapaswa kuweka namba ya kampuni 400700 na kumbukumbu namba 400700.
Akaunti ya CRDB bank, 0150021209500 jina la akaunti Data Vision International -Tuko Pamoja.




No comments:
Post a Comment