Waziri Mwijage:Ukiwa na cherehani nne unamiliki kiwanda ...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa viwanda, biashara na uwezeshaji Charles Mwijage ameendelea
kusisitiza kwamba kwa mujibu wa tafsiri ya serikali ya awamu ya tano ukiwa na cherehani nne unamiliki kiwanda.
Waziri wa viwanda, biashara na uwezeshaji Charles Mwijage katikati akiandika jambo fulani alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesisitiza hilo wakati alipotakiwa na kutoa tafasiri halisi
ya viwanda vinavyozungumziwa.
“Na hapa tuwe makini kidogo kwa sababu kuna watu wengine
wanataka kupotosha, watu wengine wanalenga kubeza na rudia kwa mara ya 26 cherehani nne kwa tafsiri yetu ya viwanda ni kiwanda kidogo,” amesema
Mwijage.
Mwijage aliombwa kutoa tafsiri hiyo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi ya maonesho ya
pili ya bidhaa za viwanda
yatakayofanyika kuanzia Desemba 7 hadi 11, 2017.
Watu wamekuwa wakikosoa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa na
waziri Mwijage kwamba tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani zaidi
ya viwanda 3000 vimekwisha jengwa huku katika takwimu hizo akitaja hata mwenye cherehani nne anakiwanda.
Pia amesema lengo ni kujenga viwanda jumuishi
vitakavyotumia malighafi za ndani badala ya nje.
Pia amesema lengo ni kujenga viwanda jumuishi
vitakavyotumia malighafi za ndani badala ya nje.




No comments:
Post a Comment