Waziri aitaka ACSAF kufikisha mawasiliano kote nchini...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
MFUKO wa mawasiliano kwa wote (ACSAF) umetakiwa kufikisha huduma ya mawasiliano kote nchini.
Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu waziri wa
ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa
habari alipotembelea mfuko huo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa
miradi ya usambazaji wa huduma ya mawasiliano.
“Mkakati wa serikali ni kuhakikisha huduma ya mawasiliano
inamfikia kila mwananchi, mnatakiwa kuharakisha huduma hii katika maeneo ambayo
bado hayajafikiwa, lakini jamii pia itoe ushirikiano pale wanapoona miradi ya
mawasiliano inatekelezwa katika maeneo yao,” amesema Nditiye.
Naibu waziri huyo amesema kwa sasa wananchi wengi wamepata
hamasa za kuhitaji mawasiliano na kusisitiza kuwa kutokana na mwamko huo juhudi
za haraka zinahitajika katika kuwafikishia huduma hiyo.
Amewataka watekelezaji wa huduma za mawasiliano
kuhakikisha wanapeleka miradi hiyo maeneo yaliyokusudiwa pekee.
"watoa huduma hakikisheni hamfania kazi ya kupindisha
miradi yaani ilipokusudiwa kupelekwa hampeleki hiyo mtakuwa hamtekelezi azma ya
serikali ya kufikisha mawasiliano kwa wote"amesema.
kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga amesema tangu waanze
utekelezaji wa miradi ya mawasiliano kwa wote wa 2013 wameshafikia zaidi ya
wananchi milioni 4.
Pia wamefikia zaidi ya vijiji 2000 na kata 444 huku zaidi ya kata 120
zikiwa katika hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.
"Kabla mfuko huu haujaanza ni asilimia 80 ya wananchi
walikuwa wamefikiwa, lakini kwa sasa imefikia asilimia 90, inamana kwamba mfuko
huu umeongeza asilimia 10 na gharama za miradi tuliyofadhili zimefikia
zaidi bilioni 85,” amesema Ulanga.
Amesema kama mfuko huu usingekuwepo zaidi ya wananchi milioni 5
wasingekuwa wamefikiwa na huduma hii.




No comments:
Post a Comment