Zitto Kabwe, Freeman Mbowe wateta...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
KIONGOZI wa Chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe amekutana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema), Freeman Mbowe kujadili mwenendo mzima wa demokrasia na vyama vya siasa nchini. 

Freeman mbowe akizungumza na Zitto Kabwe

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es Salaam Zitto anasema juzi chama hicho kilifanya kikao na kuamua kugomea ushiriki wa uchaguzi wa marudio.

Amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini.
Zitto anasema lengo la kukutana na wadau hao  ni kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu.
"Kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala cha kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini,"amesema .
Amesema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza jambo hilo huku akipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama hivyo.  
Zitto anasema tayari jana ameshazungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, James Mbatia aliye hospitali KCMC baada kupata ajali.
"Nafurahi kwamba mazungumzo yetu yameanza vizuri,"amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search