Sita wafariki, wengi wajeruhiwa DRC...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
WATU sita wamefariki na wengine kujeruhiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC)  baada ya jana polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaomtaka rais Joseph Kabila aondoke madarakani.
Joseph Kabila
Watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wamekamatwa, wakiwemo waandishi habari.
Maafisa wamepiga marufuku maandamano hayo na huduma za intaneti zimefungwa.
Jana kanisa katoliki liliwataka raia washirika katika maandamano ya amani baada ya misa ya Jumapili - wakibeba bibilia rosari na misalaba.
Maafisa wa usalama walikabiliana na maandamano hayo kwa kutumia nguvu katika miji tofuati nchini.
Katika mji mkuu Kinshasa, walinda amani wa Umoja wa mataifa wanaarifiwa kutawanywa kujaribu kuwatenganisha waandamanji na vikosi vya usalama nchini.
Kumeshuhudiwa maandamano mengi dhidi ya rais Kabila tangu muhula wake umalizike zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Congo inakabiliwa pia na mizozo kadhaa ya makundi ya kujihami, hususani katika maeneo ya mashariki na kati mwa nchi hiyo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search