Apasuka koo kwa kujizuia kupiga chafya ...soma habari kamili na matukio 360...share

Na mashirika ya kimataifa
MADAKTARI wameonya kwamba kuzuia kupiga chafya kwa kufunga pua na mdomo kunaweza kukusababishia madhara makubwa.

Madaktari bingwa wa upasuaji wakimhudumia mgonjwa aliyepasuka koo



Hii inajiri baada ya madaktari mjini Leicester nchini Uingereza
kumtibu mtu mwenye umri wa miaka 34 ambaye alipusuka koo kwa kujaribu kujizuia kupiga chafya.

Huku kukiwa hakuna nafasi ya hewa ya chafya hiyo kutoka, ililazimika kupasua tishu laini.

Licha ya kwamba kisa hicho sio cha kawaida, madaktari wameonya kwamba watu wengine wanafaa kujua kuhusu hatari hiyo.

Kuzuia kupiga chafya kunaweza kuharibu masikio mbali na kuathiri ubongo wameonya katika jarida la BMJ.

Mtu huyo anasema kuwa alihisi kuwashwa katika koo yake baada ya chafya hiyo na muda mchache baadaye akaanza kuhisi uchungu na akaanza kushindwa kula na kuzungumza.

Wakati madaktari walipomchunguza waligundua kwamba alikuwa ana uvimbe katika koo na shingo yake.

Picha za X ray zilizopigwa zilibaini kwamba kuna hewa inayotoka kupitia tishu laini zilizopasuka kupitia shingo yake.

Mtu huyo alilazimika kulishwa kwa kutumia paipu kwa siku saba mfululilizo ili kutoa fursa kwa tishu hizo kupona.

Baada ya kulazwa hospitalini kwa juma moja, mtu huyo alienda nyumbani ambapo alipona.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search