Hatma ya malipo watumishi waliondolewa serikalini mwezi April ...soma habari kamili na matukio 360...share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


HATMA ya wafanyakazi waliotolewa kazini kutokana na vyeti visivyo halali 'fake' kulipwa au kutolipwa mafao yao itajulikana mwezi Machi au Aprili, 2018 kabla ya Bajeti.

 Katibu mkuu wa TUCTA, Dk. Yahya Msigwa (katikati)  akizungumza Dar es Salaam leo kuhusu majibu ya serikali kwa hoja za wafanyakazi nchini.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Dk. Yahya Msigwa wakati akizungunza na waandishi wa habari kuelezea majibu ya Serikali kwa hoja za wafanyakazi nchini.


Amesema Shirikisho limekiri kufahamu watumishi hao kufanya kosa la jinai na la nidhamu na kwamba wanawapigia magoti serikali ili wafanyakazi hao wasiondoke mikono mitupu.


"Tulitaka tufanye kiubinadamu ili hawa watu wasitoke mikono mitupu... Walau walipwe haki zao fulani,"amesema.


Amesema serikali imewajibu kuwa wapo kwenye mchakato Na mamlaka mbalimbali zinazohusika na masuala hayo zinamalizia kulifanyia kazi na kwamba  kati ya mwezi Machi au Aprili, 2018 ufumbuzi wa suala hilo utapatikana


Akizungunzia suala la wafanyakazi walioishia darasa la saba, Dk. Msigwa amesema serikali imekiri utekelezaji wake kuwa na changamoto.


"Bado kuna baadhi ya ajira inahitaji darasa la saba...baadhi yao wanaweza kurudi na baadhi wanaweza kupoteza ajira lakini hawajafanya kosa la jinai malipo ni haki yao watalipwa fedha zao na suala lao linashughulikiwa watalipwa Machi au Aprili, "amesema.


Ameongeza kuwa watumishi wengi hawajapandishwa madaraja kwa muda mrefu kutokana na mchakato wa uhakiki nakwamba serikali imeshatenga fedha za upandishwaji madaraja.


Akizungunzia madeni ya wafanyakazi, Dk. Msigwa amesema serikali imeshatenga fedha nakwamba ilisimamisha mchakato huo ili kupisha uhakiki wa madeni hayo kwani wapo waliopeleka madeni ambayo si sahihi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search