Baraza jipya la mawaziri Kenya latangazwa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameanza kuunda baraza jipya la mawaziri kwa kuwateua tena mawaziri sita wa zamani ikiwa ni miezi miwili baada ya kutetea nafasi hiyo ya urais.
Rais Uhuru Kenyatta
Akitangaza sehemu ya baraza lake jipya, rais huyo wa Kenya pia amependekeza wanasiasa wawili kuchukua nafasi za uwaziri.
Kinachoshangaza wadadisi wa maswala ya kisiasa ni kutangazwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya, KeriakoTobiko kuwa waziri.
Hii ni mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kutangaza kwamba amekubali maombi ya Tobiko ya kujiuzulu kama Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya.
Waliorejea katika baraza hilo jipya ni Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiangi, Waziri wa fedha, Henry Rotich, Waziri wa Utalii, Najib Balala, na Joseph Mucheru wa Waziri wa Teknolojia na Habari. Waziri wa Mawasiliano amesalia kuwa James Macharia na Waziri wa Kawi ni Charles Keter.
Wanasiasa walipoendekezwa na rais kushikilia wadhifa wa uwaziri ni aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Turkana ,John Munyes na aliyekuwa Govana wa Marsabit , huko Mashariki mwa Kenya, Ukur Yatani.
Kiongozi huyo wa Kenya anayehudumu kwa kipindi chake cha pili na cha mwisho kama rais amesema bado yuko katika harakati ya kubuni baraza lake kamili .
Katiba ya Kenya inasema kwamba baraza la mawziri sharti liwe na mawaziri kati ya 14 na wasizidi 22.
Rais Uhuru Kenyatta aliingia madarakani kwa awamu ya pili baada ya kutangazwa mshindi wa urais baada ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya mwezi Oktoba mwaka 2017.




No comments:
Post a Comment