UPDATES: Tundu Lissu aondoka kwenda Ubelgiji....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu

MWANASHERIA mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu mapema asubuhi ya leo ameondoka kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu ya viungo.

Tundu Lissu akitoka hospitali jijini Nairobi Kenya kuelekea uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kwenda nchini Ubelgiji

Jioni Jana akizungumza na matukio360, Lissu alisema fedha za matibabu zinagharamiwa na wadau wa vyama vya upinzani na marafiki mbalimbali.

"Nashukuru Mungu inaendelea vizuri lakini ninakwenda Ubelgiji kwa matibabu ya viungo kwani mtu ilikata muda mrefu unapoteza uwezo wako wa kawaida wa kutembea. Fedha za matibabu zinagharamiwa na wadau wa vyama vya upinzani na marafiki mbalimbali," alisema

Septemba 7, 2017 Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashirika alipigwa risasi mjini Dodoma alipokuwa anahudhuria vikao vya Bunge la Tanzania. Amelazwa katika hospitali mjini Nairobi kwa takribani miezi minne.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search