CUF Lipumba 'walia' rafu uchaguzi Kinondoni...soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
CHAMA cha Wananchi CUF upande unaomuunga mkono Mwenyekiti
Profesa Ibrahim Lipumba umemteua Rajab Juma aliyekuwa kampeni meneja wa Maulid
Mtulia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni CUF Lipumba, Rajab Juma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu.
Pia mgombea huyo amelalamikia kitendo cha Mtulia anayegombea
tena ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kampeni.
Malalamiko hayo ameyatoa leo akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye ofisi za halmashauri ya manispaa ya
Kinondoni.
amesema Mtulia ameanza kupita katika matawi ya CUF kuomba kuungwa mkono.
amesema Mtulia ameanza kupita katika matawi ya CUF kuomba kuungwa mkono.
“Tumeshasainiwa fomu, isipokuwa kuna mambo ya kusikitisha
sana, na sisi kama wanasiasa tumeona tuanze mapema kutoa angalizo ili muweze
kutusaidia, sasa mgombea wa CCM ameanza kupita katika matawi yetu ya CUF,kwanza
kipindi cha kampeni bado lakini ni makosa kwa mgombea wa chama kingine kwenda
katika chama chetu,” amesema Juma.
Amesema suala hilo kama halitachukuliwa hatua litaleta athari
kwani siasa siyo chuki,uadui na wamedhamiria kufanya siasa kama sehemu ya
kuweza kuondoa kero ambazo zinawakabili wananchi.
Mkurugenzi wa habari na Uenezi wa CUF Lipumba, Abdul Kambaya amesema
kitendo cha CCM kumteua Mtulia kuwa mgombea wao inadhihirisha kwamba kimeridhia
matumizi mabaya ya fedha za umma.
“Alichokifanya Mtulia ni kutuitisha kwenyae uchaguzi mdogo
usiokuwa na sababu, hakufa ni mzima, haumwi, hana tatizo la kutohudhuria
bungeni, ameamua kujizulu uanachama na kupoteza nafasi ya ubunge na uchaguzi ni
gharama fedha za walipakodi wa Tanzania zinakwenda kutumika kwenye uchaguzi
mdogo usiokuwa na sababu,” amesema Kambaya.
Ameongeza kuwa
wanauhakika watashinda katika uchaguzi kwa kuwa wanamgombea mzuri, uwezo na mwenye kujiamini.
Uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la kinondoni unatarajiwa
kufanyika Februari 17, 2018 na unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo Maulidi Mtulia kujiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM kwa madai kwamba
ni kuunga juhudi za Rais John Magufuli katika kupigania rasilimali za taifa
ampapo kwa sasa pia ni mgombea kupitia chama hicho.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kindondoni CUF Rajab Juma akikabidhiwa fomu na msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni Latifa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment