Serikali yatahadharisha matumizi holela ya dawa za Antibiotiki ....soma habari kamili na matukio 360...#share

Na Salha Mohamed,Dar es Salaam


SHIRIKA la Afya duniani (WHO), limetoa maelekezo kwa Serikali kutumia kwa umakini mkubwa dawa za antibiotiki ili kudhibiti kuenea kwa usugu wa vimelea vya magonjwa ya kuambukiza.


 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa nakala ya muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa muhimu, hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam

Hayoyamebainishwa Dar es Salaam leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizindua Muongozo wa Matibabu nchini na orodha ya taifa ya matumizi ya Dawa Muhimu.


Amesema muongozo huo wa tano kutolewa, umezingatia kuimarisha huduma katika ngazi za Zahanati na Vituo vya Afya ambapo dawa ambazo hazikuwepo kwenye muongozo wa awali sasa zimeainishwa.


"Baadhi ya dawa hizi ni zile za katibu magonjwa ya Kisukari, Ukimwi, Kifua kikuu, Malaria... Wizara itaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa kuajiri wataalam wenye ujuzi stahiki, "amesema.


Amesema katika muongozo huo, dawa za antibiotiki zimegawanywa katika makundi matatu ya 'ACCESS', 'WATCH'   na 'RESERVE'.


"Atibiotiki za kundi la kwanza zimeainishwa kutumika katika ngazi zote za kutolea huduma nchini, antibiotiki kundi la pili haziruhusiwi kutumika ngazi ya zahanati na vituo Afya bali zitatumika katika ngazi ya hospitali za halmashauri, "amesema.


Ameongeza kuwa Antibiotiki kundi la tatu zitatumika katika ngazi ya hospitali za rufaa za kanda, hospitali ya taifa na hospitali maalum.


"Nasisitiza tuzingatie mgawanyo huu pale tunaponunua au kuagiza dawa Bohari Kuu ya Dawa ( MSD), "amesema.


Amefafanua kuwa, matumizi ya muongozo huo wa matibabu na orodha ya taifa ya dawa utarahisisha ununuzi wa dawa kwa MSD  kwani vituo vya vituo vya kutolea huduma vitaweza kufanya makadirio ya manunuzi ya dawa na kuimarisha upatikanaji wake katika vituo vya kutolea huduma.


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Mohamed Bakari Kambi amewataka wataalam kuwa mstari wa mbele kutumia muongozo huo na kutoa mapungufu wizarani ili kuboresha.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search