David Beckham kuitangaza rasmi timu yake....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
MCHEZAJI wa zamani  wa timu ya mpira wa miguu wa nchini Uingereza, David Beckham amefanikiwa mpango wake wa muda mrefu wa uzinduzi wa timu yake ya soka huko Miami.
David Beckham
Timu hiyo haijatajwa mpaka sasa ingawa inatarajiwa kucheza mbele ya umati wa watu elfu ishirini na tano mjini Overtown na katika viwanja vilivyoko karibu na mji huo.
"Ninafuraha kubwa kuileta timu hii kubwa kwenye jiji hili kubwa, ilikuwa ni safari ndefu na ngumu mpaka kufikia hapa nilipo leo anasema kiungo wa zamani wa timu ya Manchester United Beckham, mwenye umri wa miaka 42.Nina waahidi itakwenda katika ligi ikiwa ni timu bora anajinasibu David.
Baada ya uzinduzi huo David Bekham alipongezwa na watoto wake wanne kwa njia ya video maalum akiwemo mkewe Victoria, ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki wa zamani wa kundi la Spice Girl , miongoni mwa waliohudhuria ni mshindi mara 23 wa michuano ya Grand Slam, Serena Williams, mshindi mara nane wa medali ya dhahabu wa michuano ya Olimpic, Usain Bolt na watu wengine maarufu akiwemo Brady, Will Smith, Jay Z na Jennifer Lopez.
Beckham alijiunga na timu ya LA Galaxy akitokea timu ya Real Madrid mnamo mwaka 2007 na kuwa mchezaji wa kwanza mstaafu kumiliki timu katika ligi.
Anajinasibu David kuwa alijiunga na timu ya Galaxy kwasababu alitambua uwezekano wa kudumu kwa muda mrefu katika ligi hii, "alisema.
Niliamua kuondoka Real Madrid na kwenda kwenye ligi ambayo ilikua inasuasua, ilikuwa ni hatua kubwa mno niliyopiga na kitu kimoja ninachokijua ni kuwa hatua hiyo itazaa matunda yenye changamoto lakini changamoto zenye kusisimua.
Kamishna Garber alikuja akaketi karibu yangu na kuanza kunieleza mipango ya ligi na wapi anapotaka kuifikisha nilikuwepo tangu siku ya kwanza.
Uzinduzi huu haikuwa kazi rahisi kwa muda wa miaka minne ya utafutaji kiwanja eneo la kusini mwa Florida huku tukipingwa na baadhi ya watu katika maeneo kadhaa.
Washirika wa David Beckham walinunua ardhi tayari kwa kujenga uwanja wao mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, baada ya kushindwa mara tatu kununua eneo walilolitaka na bora zaidi kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Miami ilifikishwa mahakamani na mfanyabiashara tajiri Bruce Matheson, aliyedai kuwa timu ya Beckham ilinunua ardhi haikununua kwa gharama stahiki na zabuni isiyokuwa na ushindani bila kufuata utaratibu. Madai hayo yalitupiliwa mbali, ingawa mfanya biashara huyo Matheson ameapa kukata rufaa.
Washirika wa Beckham ni pamoja na meneja wa zamani wa kundi la Spice Girls Simon Fuller, Mfanya biashara mwenye asili ya Bolivia na Marekani Marcelo Claure, Mfanya biashara kutoka Florida Kusini Jorge , Jose Mas na Mjasiriamali wa Kijapani JMasayoshi Son.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search