DSE:Ukubwa mtaji kampuni za ndani wapungua.....soma habari kamili na matukio360...#share


Na Salha Mohamed, Dar es Salaam 

UKUBWA wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko la hisa umepungua kwa sh.  Bilioni 159 kutoka sh.  Trilioni 22.9 wiki iliyopita hadi ah. Trilioni 22.9 wiki iliyoishia Januari 26,2018. 
Mary Kinabo

Punguko hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni ya Vodacom kwa asilimia 13,National Media Group (NMG)kwa asilimia 8 na Acacia (ACA) kwa asilimia 2.

Taarifa ya DSE iliyotolewa leo inasema, ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kwa sh. Bilioni 217 kutoka sh. Trilioni 10.3 hadi kafika sh. Trilioni 10.1 wiki hii.

Inasema kupungua kutokana na kushuka kwa bei ya hisa ya VODA kwa asilimia 13%.

Mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia Januari 19, 2018 yalikuwa sh. Bilioni 1.8 na wiki iliyoishia Januari 26, 2018 yakawa sh Bilioni 44.6.

Vile vile Idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia Januari 19,2018 zilikuwa hisa milioni 1.96 na wiki iliyoishia Januari 26,2018 idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni  ilikuwa hisa milioni 5.5. 

Aidha kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 16 kutoka pointi 2,377 hadi 2,360 pointi kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Vodacom Tanzania Plc (VODA), National Media Group (NMG) na Acacia (ACA).

Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeshuka kwa pointi 83 kutoka pointi 3,936 hadi pointi 3,853 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Vodacom.

Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 5,504.

Pía, Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa pointi 38 kutoka pointi 2,517 kadi pointi 2,555 hii imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 10 kutoka sh 1340 hadi 1480 na CRDB kwa asilimia 6 kutoka sh. 175 hadi sh.185.

Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imeshuka kwa pointi 288 kutoka pointi 2,172 hadi pointi 2,473 imechangiwa na kushuka kwa bei za hisa za VODA kwa 13 kutoka sh 850 hadi  sh 740.

Aidha mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Januari 26,2018 yalikuwa sh. bilioni 23 kutoka sh. milioni 522 wiki iliyopita ya Januari 19,2018.  

Mauzo hayo yalitokana na hatifungani kumi na tatu za serikali zenye jumla ya thamani ya sh.  bilioni 25 kwa jumla ya gharama ya sh. bilioni 23.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search