Shughuli za kiuchumi, kijamii zaathiri mazingira nchini...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI imesema kasi ya ukuaji wa uchumi na kupanuka kwa
shughuli za kijamii inasababisha kuongezeka kwa changamoto za masuala ya
uhifadhi wa mazingira na usimamizi sahihi na endelevu kwa rasilimali nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Faustine Kamuzora alipokuwa akizindua warsha ya
wadau kuhusu upatikanaji wa takwimu za kupima na kutathmini utekelezaji wa
mpango wa pili wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano na viashiria vya malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) katika sekta ya mazingira na matumizi endelevu ya
rasilimali.
Kutokana na changamoto hiyo, Prof. Kamuzora amesema serikali imefanya
jitihada kuweka mfumo wa kisheria na kitaasisi ili kudhibiti huhifadhi wa
mazingira ikiwa ni pamoja na kuingiza masuala hayo kwenye sera ya mipango ya
maendeleo kitaifa.
“Kutokana na changamoto zinazosababishwa na kasi ya ukuaji wa
uchumi na kupanuka kwa shughuli za kijamii serikali imefanya jitihada kubwa
katika kuweka mfumo wa kisheria na kitaasisi katika kudhibiti masuala ya
uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuingiza masuala ya mazingira kwenye
sera ya mipango ya maendeleo ya kitaifa,” amesema Prof. Kamuzora
Ameongeza “ kunajitihada mbali mbali kama mnavyofahamu, kuna
sera yazamani kidogo ya 1997 ambayo kwa sasa imehuishwa kuwa ya mazingira na kunasheria ya mazingira ya mwaka 2004 yenyewe
ishafanyiwa marekebisho kidogo."
Akizungumzia warsha hiyo, amesema kuwa anaamini wadau hao
watakuja na jibu la jinsi ya kutumia mazingira na rasilimali vizuri kwa ajili
ya maendeleo endelevu.
Prof. Kamuzora ameongeza kuwa katika mpango wa maendeleo wa
miaka mitano masuala ya mazingira yamewekwa ili kuhakikisha mazingira hayaathiriwi
kwa namna yoyote ile.
Ameeleza kuwa Ofisi ya
Takwimu (NBS) kwa kushurikiana na wadau mbali mbali wameunda kamati tendaji
ambayo inahusisha sekta binafsi, umma na asasi za kiraia kuhakikisha kwamba
hakuna mtu anayeachwa nyuma katika suala la uhifadhi wa mazingra.
No comments:
Post a Comment