Halmashauri zatakiwa kushirikiana na mashirika ya kidini....soma habari kamili na matukio360...#share





Na mwandishi wetu Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewaagiza wakurugenzi na wakuu wa halmashauri zote kushirikiana kikamilifu na hospitali za mashirika ya kidini katika utoaji huduma za afya na kuhakikisha kunakuwepo na dawa za kutosha.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifungu mkutano wa kusaini mikataba ya utoaji huduma kwa Halmashauri tano na hosptali za mashirika ya kidini kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo ya Ujerumani(GIZ).




Ametoa agizo hilo leo jijini hapa wakati wa kusaini mikataba ya
utoaji wa huduma ya pamoja baina ya halmashauri tano za mkoa na hospitali binafsi ili kutekeleza azma ya serikali kuboresha huduma ya afya katika jamii kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) .




"Mkataba huu ukawe chachu katika utoaji huduma ya afya katika jamii pia watumishi serikalini tatueni kero za viongozi wa dini na si kusubiri mpaka kuibuke migogoro mikubwa ambayo inajenga taswila mbaya katika mkoa,"amesema.




Amesema ni jukumu la kila halmashauri kutanguliza uzalendo wa nchi mbele kwa kusikiliza kero za wananchi hususan mpango mkakati wa kuboresha huduma za afya za msingi kwa kushirikiana na pande zote mbili.




Amesema uwepo wa mkataba huo utakuwa chachu katika kuondokana na changamoto walizokuwa wakikumbana nazo wananchi hususan kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya .




Makalla amesema ni wajibu wa kila halmashauri kushirikiana na sekta binasfi kwa kuwa zinachangia asilimia 14 katika utoaji wa huduma ya afya na kwamba mikataba hiyo isiwe ya vificho na iwe ya wazi






Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Mbeya, Yahya Msuya amesema mpango huo ni chachu ya utoaji wa huduma kwa wanawake na watoto na kuomba waganga wakuu wa kila halmashauri kusimamia mradi huo.




Katibu Tawala Mkoa Mariam Mtunguja amesema katika kusimamia mradi huo serikali itahakikisha kunakuwepo kwa madawa ya kutosha na wataalam watakao saidia na hospitali za mashirika ya kidini ili kuboresha sekta hiyo muhimu.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search