Matokeo kidato cha nne hisabati, fizikia, biashara, mahesabu bado kitendawili!...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


BARAZA La Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato nne (CSEE) na maarifa (QT), ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba, wavulana wakiongoza huku somo la hisabati, fizikia, commerce na Book keeping wanafunzi hawakufanya vizuri

Dk Charles Msonde

Mtihani huo ulifanyika Oktoba hadi Novemba, 2017 katika shule 4,786 jumla ya watahiniwa 385,767 walisajiliwa ,wasichana wakiwa 198,036 sawa na asilimia 51 na wavulana wakiwa 187,731 sawa na asilimia 48.66.


Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji,Dk Charles Msonde amesema ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo ya Civis, Historia, Geografía, Kiswahili, English, Biology, Hisabati, na commerce umepanda kwa asilimia 1.07 na 9.85 ukilinganishwa na mwaka 2016.


Ametaja shule kumi bora kuwa ni St. Francis Girls ya Mbeya, Feza Boys ya Dar es Salaam, Kemeboys ya Kagera, Bethel Sabs Girls ya Iringa, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Mariani Girls ya Pwani, Canossa ya Dar es Salaam, Feza Girls ya Dar es Salaam, Marian boys ya Pwani na Shamsiye boys ya Dar es Salaam.


Aidha, Dk Msonde amezitaja shule kumi za mwisho kitaifa kuwa ni Kusini ya Kusini Unguja, Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja, Mwenge  S. M. Z ya Mjini Magharibi, Langoni ya mjini magharibi, Furaha ya Dar es Salaam, Mbesa ya Ruvuma, Kabugaro ya Kagera, Chokocho ya Kusini Pemba, Nyebuku Dar es Salaam na Mtule ya Kusini Unguja.


"Pamoja na kuwa ufaulu umeendelea kuimarika, takwimu zinaonesha bado ufaulu wa masomo ya physics, Hisabati, Commerce na Book Keeping upo chini ya asilimia 50,hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuinua kiwango cha ufaulu, "amesema.


Amesema jumla ya watahiniwa 265 wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu huku mtahiniwa mmoja kuandika matusi katika karatasi yake ya majibu ya mtihani.


"Watahiniwa 136 wa kujitegemea walifanya udanganyifu na watahiniwa 129 wa shule walikamatwa na vitu visivyoruhusiwa ndani ya chumba cha mtihani kama simu, notes, vitabu wakati mtihani ukiendelea walikuwa watahiniwa 123, "amesema.


Amefafanua kuwa watahiniwa 62 walibadilishana skript, namba na kuwa na miandiko tofauti, watahiniwa 73 walikutwa na mfanano wa majibu ya kukosa na usio wa kawaida huku watahiniwa 7 wakiwafanyia mtihani watu wengine.


Amesema wamezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo  na kupewa fursa ya kufanya masomo mitihani ambayo hawakufanya mwaka 2018.


Amefafanua kuwa watahiniwa 77 wa shule walipata matatizo kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote ambapo wamepewa fursa ya kufanya mtihani mwaka 2018.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search