Jengo la kisasa la upasuaji hospitali Mwananyamala lazinduliwa....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda  amezindua Jengo la Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es salaam lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 420.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika picha ya pamoja na watendaji wa hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kuzindua jengo jipya la upasuaji

Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa moja litasaidia kupunguza idadi ya vifo mama na mtoto limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE Kama sehemu ya kuenzi jitiada za Makonda katika kuboresha Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.


Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo March 13 siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia wagonjwa 20 kwa siku.


Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha maumivu makali na vifo vya mama na mtoto lakini kupitia jengo hilo vifo vitapungua.


Makonda ameishukuru kampuni ya GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa jengo hilo ambapo inakadiriwa hospitali hiyo inapokea wagonjwa kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na miongoni wakiwa ni wajawazito wanaohitaji huduma ya Upasuaji.


Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua salama ndani ya jengo hilo na linaendelea kupokea wajawazito kila kukicha.


Baadhi ya wakiinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru Makonda kuwajengea jengo hilo la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya kazi yao pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji zikienda vema.


Viongozi waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya ya kinondoni,  Mstahiki Meya wa Kinondoni,watendaji wa Afya na wananchi wamempongeza Makonda kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha sekta ya Afya mkoani humo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search