Dawa za kuongeza nguvu za kiume zazua balaa....soma habari kamili na matukio 360...#share

Na mashirika ya kimataifa
WANAUME watatu nchini Zambia wamelazwa kwa makosa katika wadi ya wagonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Wanaume hao watatu wanatoka katika mji mdogo wa katete, na si wagonjwa wa kipindupindu bali walikunywa dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa inayojulikana kama Mvubwe.

Watu waliokunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume wakiwa wamelazwa wakipatiwa matibabu
Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo amesemaa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili.
''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa''
Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hicho cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza  Kasolo.
Ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mwaka jana ulisababisha vifo vya watu takribani 70, kusini mwa Afrika.
Rais Edgar Lungu mwezi uliopita, alitoa agizo kwa jeshi la Zambia kusafisha maeneo ya masoko na kuondoa uchafu ambao ndio sababu ya kipindupindu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search