Jinsi sigara inavyosababisha ugonjwa wa moyo, kiharusi....soma habari kamili na matukio 360...#share

Na mashirika ya kimataifa
KWA mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la utafiti wa masuala ya afya la BMJ, wavutaji sigara wanahitaji kuacha kabisa kuvuta badala ya kupunguza uvutaji ili kuepuka hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi.

Watu wanovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 50 zaidi kupata magonjwa ya moyo na wanauwezekano wa asilimia 30 wa kupatwa na kiharusi kuliko watu amabo hawajawahi kuvuta sigara,watafiti wamesema.
Wamesema inaonesha kuwa hamna kiwango salama cha uvutaji wa sigara kwa magonjwa hayo na kwamba wanawake wako katika hatari zaidi - asilimia 57 wanaweza kupata ugonjwa wa moyo na asilimia 31 kupata kiharusi
Lakini wataalam wamesema watu wanaopunguza uvutaji wanauwezekano mkubwa wakuacha tabia hiyo kabisa
Asilimia 48 ya vifo vya mapema vinavyohusiana na uvutaji wa sigara hutokana na ugonjwa wa moyo
Wakati idadi ya watu wazima wanaovuta nchini Uingereza imekuwa ikishuka, idadi ya watu wanaovuta sigara moja hadi tano kila siku imeendelea kupanda,watafiti hao wamesema.
Utafiti huo umesema kuwa wanaume wanaovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 48 wa kupata ugonjwa wa moyo na wanauzekenao wa asilimia 25 wa kupatakiharusi kuliko wale ambao hawajawahi kuvuta kabisa.
Profesa Allan Hacksaw wa taasisi ya saratani UCL katika chuo cha College London amesema ongezeko la hatari ya magonjwa ya moyo yapo katika kipindi cha muda mrefu lakini uharibifu waweza fanyika katika kipindi cha miaka michache tu.
Lakini ameongezea kuwa habari njema ni kwa wale watakao acha kabisa kuvuta sigara wanaweza kupunguza kwa haraka zaidi hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search