Kampuni ya Robert Mugabe kushtakiwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

KAMPUNI moja ya rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe inatakiwa kuondoka katika kipade kimoja cha ardhi kinachomilikiwa na shule moja la sivyo ishtakiwe.
Robert Mugabe
Kampuni hiyo kwa Jina Gushungu Holdings inadaiwa kunyakuwa kipande hicho cha ardhi chenye ukubwa wa hekari 23 katika eneo moja la makazi ya mji wa Harare.
Kanisa la Reform linasema kuwa ardhi hiyo inamilikiwa na kundi la shule zake la Eaglesvale.
Wakili wa shule hiyo Rodney Makausi amesema mwaka 2016 serikali ilichukua ardhi hiyo kwa nguvu.
Serikali baadaye ikaondoa madai yake baada ya swala hilo kuwasilishwa mahakamani.
Lakini mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Enos Chomutiri anasema kuwa mahindi yalipandwa katika shamba hilo mwaka uliopita na bango kubwa la shule hiyo likaondolewa.
Mawakili wametaka kampuni hiyo kuondoka katika shamba hilo mwisho wa mwezi huu ama ishtakiwe.
Sio mara ya kwanza familia ya Mugabe imetuhumiwa kuchukua mali kwa nguvu.
Awali, familia hiyo imekuwa na mgogoro na wakulima masikini kuhusu ardhi moja inayodaiwa kuwa na utajiri wa dhahabu ,pia familia hiyo imetuhumiwa kwa kunyakua shamba moja linalozalisha ndimu zinazouzwa nje ya taifa katika eneo hilo hilo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search