Mikoa kumi wilaya 20 inakabiliwa na ugonjwa wa ukoma...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
SERIKALI imesema mikoa kumi na wilaya 20 bado inakabiliwa na maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukoma.
Mikoa hiyo ni Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani, Tanga, Geita, Dodoma, Tabora na Kigoma na wilaya ni Liwale Nkasi, Ruangwa, Nanyambu, Shinyanga Manispaa, Kilombero, Mafia, Pangani, Mvomero, Masasi mjini, Lindi vijijini, Kilwa, Mpanda, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Mkinga, Ulanga, Morogoro vijijini na Chato.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk Faustine Ndugulile (katikati) akitoa tamko leo jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya ukoma duniani Januari 28,2018 (kushoto) Mkurugenzi wa Kinga wizarani hapo, Dk. Neema Rusibamayila na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya ukoma duniani Januari 28 yenye kauli mbiu 'Tokomeza ukoma kuzuia ulemavu miongoni mwa vijana wetu'.
"Pamoja na kwamba nchi yetu ilifikia viwango vya utokomezaji wa ukoma kitaifa mwaka 2006 kwa kiwango cha chini ya mgonjwa 1 kati ya 10,000... Ukoma bado unaendelea kuwa tatizo la kiafya miongoni mwa jamii nchini kwetu, "amesema.
Amesema kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na ukoma za mwaka 2016, wagonjwa wapya 2,047 waligunduliwa na kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu 4 kwa kila watu 100,000.
"Takwimu hizi zinaifanya Tanzania kuendelea kuwa miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa ukoma duniani, "amesema.
Dk. Ndugulile amefafanua kuwa mwaka 2007 hadi 2017 takwimu zinaeleza watoto 1,456 waligunduliwa na kutibiwa ukoma miongoni mwao,watoto 73 waligunduliwa wakiwa wamepata ulemavu wa kudumu kwa kukatika baadhi ya viungo vyao na kutumia viungo bandia na kuwa tegemezi katika maisha yao.
"Dalili za awali za ukoma ni baka au mabaka kwenye ngozi yasiyo na hisia na yenye rangi ya shaba, mguso au maumivu, vijinundu (vijifundo) kwenye ngozi hasa usoni na masikioni.
"Uvimbe na maumivu kwenye mishipa ya fahamu, ganzi kwenye mikono au miguu, vidonda au kuungua moto katika mikono na miguu bila kusikia maumivu yoyote, "amesema.
Amesema athari za kuchelewa kwa mgonjwa kupata matibabu ni kukatika vidole vya mikono,miguu na upofu.
Amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa huku jamii ikiendelea kishikilia imani potofu kuwa ugonjwa huo ni wa kurithi au kulogwa na wagonjwa kuchelewa kupata tiba hadi atakapopata ulemavu.
"Ukoma unatibiwa bure... Ni ugonjwa wa kuambukizwa kwa njia ya hewa unasababishwa na vimelea vinavyoshambulia mishipa ya fahamu viitwavyo Myco Bacteria Leprae, tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na watoto wetu na kwenda hospitali unapoona dalili za ukoma, "amesema

No comments:
Post a Comment