Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi...soma habari kamili na matukio 360...#share


Na mashirika ya kimataifa

Mkataba wa Manchester United kumsaini mshambualiaji wa Arsenal raia wa Chile,Alexis Sanchez utagharimu pauni milioni 180 baada ya Sanchez kukubali mkataba wa miaka minne na nusu. (Telegraph)

Alexis Sanchez

Mkataba wa Sanchez na Manchester United utamlipa mchezaji huyo wa umri wa miaka 29, paunia 400,000 kwa wiki. (Independent)

Liverpool wamewaambia Sevilla kuwa hawako tayari kumnunua mshambuliaji raia wa England Daniel Sturridge, 28 kwa mkopo. (Mail)

Mchezaji anayemezewa mate na Chelsea Andy Carroll aliiambia West Ham kuwa hawezi kufanya mazoezi - lakini klabu hiyo inauliza ni kwa nini licha ya mchezaji huyo kufanyiwa uchunguzi kwenye goti lake. (Mirror)


Meneja wa West Ham David Moyes alikuwa Stamford Bridge siku ya Jumatano kumtazama mshambuliaji raia wa Ubelgi Michy Batshuayi, ambaye anataka kumsaini. (Mail)

Real Madrid wanaamini kuwa wakati umewadia kuwasaini washambuliaji watatu wakiwemo mshambuliji wa PSG raia wa Brazil Neymar, Eden Hazard wa Chelsea na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.(Marca)




Bayern pia huenda wakazungumza na Everton kuhusu beki raia wa Uhispania Juan Bernat. (Liverpool Echo)

Mwekezaji mkuu raia wa Uingereza ambaye alikuwa na mpango wa kumsaidia Amanda Staveley kuinunua Newcastle sasa ameamua kuunga mkono ununuzi huo. (Guardian)

Meneja wa Newscastle Rafael Benitez atafanya hatua mpya ya kumshawishi mmliki Mike Ashley kufadhili ununuzi wa wachezaji wapya mwezi Januari.(Northern Echo)

Liverpool wana hofu kupoteza kwa Bayern Munich mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka, 22. (Liverpool Echo)

Mlinzi wa Arsenal Hector Bellerin huenda akawa lengo la Juventus msimu huu. Juventus wamekuwa wakimtazama mchezaji huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania tangu mwaka 2014. (Tuttosport - in Italian)

Juventus pia wanamtafuta mchezaji wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, 25, au kiungo wa kati mjerumani Mesut Ozil kuwa nambari 10 wao mpya. (Corriere dello Sport - in Italian)

Chelsea wamejiunga na Manchester City na Paris St-Germain katia mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Nice raia wa Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search