Msikie Humphrey Polepole kuhusu Ukawa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Humphrey
Polepole amedai kuwa kuanzishwa kwa Ukawa ilikuwa ni mpango mkakati wa Chadema
kuvitumia vyama vingine.
Humphrey Polepole
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Polepole amesema kuwa kwa sasa Ukawa
haupo na kilichobaki ni Ukiwa.
Amesema “Hakuna kitu kinaitwa Ukawa, hii ilikuwa project ya Chadema ikivitumia
vyama vingine, CUF, NCCR na NLD. Kilichobaki ni Ukiwa, katika jimbo lililokuwa la CUF leo CDM na CUF wanamenyana.
Wazee wa Ufipa
wala hawajali maana ni #WajasiramaliSiasa
wale, Zindukeni.”
Chimbuko la ukawa ilikuwa ni kipindi kile cha mchakato wa
mabadiliko ya katiba. Hivyo baadhi ya vyama vya upinzani viliungana kwa madai
kuwa ni kupigania maslahi ya wananchi kupitia Katiba mpya.
Vuguvugu hilo liliviunganisha vyama hivyo hadi kushirikiana
katika uchaguzi wa wabunge, udiwani na urais mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment