Waziri aagiza mkandarasi afukuzwe ....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu-SONGWE.
NAIBU Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Said Ilando kumchukulia hatua za kisheria na kumtoa katika nafasi hiyo, Mkandarasi kituo cha Afya Tunduma Sospeter Lutonja, kutokana na matumizi mabovu ya fedha zilizotolewa za ujenzi wa thieta, wodi ya kujifungulia, chumba cha mama na mtoto, Maabara, Mochwari na Nyumba ya watumishi.
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri matibabu katika Kituo cha Afya cha Mbozi Mkoani Songwe katika
Amebainisha hayo leo akiwa katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Songwe katika Halmashauri ya mji wa Tunduma ya Kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa katika vituo vya Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kushiriki shughuli za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa vituo vya Afya.
Dk. Ndugulile amesema kwamba Mkandarasi huyo hafai kuendelea na ujenzi wa kituo hicho kwasababu ya kutokidhi viwango vya ubora na kufanya urasimu katika fedha ya umma kwa kuitumia vibaya huku majengo aliyojenga kukosa ubora.
“Mnafanya mchezo na fedha za Serikali, tutawafunga nawaambia, fedha tulizotoa ni kwaajili ya ujenzi wa Thieta, Wodi ya kujifungulia, Chumba cha mama na Mtoto, Maabara, Mochwari na Nyumba ya watumishi tu, nyie mnaenda kujengea ukuta, nawaambieni tutawafunga” amesema Dk. Ndugulile kwa jazba.
Mkandarasi huyo amekwisha tumia zaidi ya sh milioni 100 kukarabati nyumba ya mtumishi, ilioonekana kuwa na kasoro nyingi licha ya kumalizika na kujenga msingi wa thieta nao ukionekana kuwa na kasoro nyingi huku akishindwa kutumia ramani katika ujenzi wa majengo hayo.
Dk. Ndugulile ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kumwandalia taarifa ya mipango ya matumizi ya pesa hiyo ambayo ni sh milioni 500, na kuwaonya wakishindwa kufanya hivyo atazichukua pesa hizo na uzielekeza katika Halmashauri nyingine zenye uhitaji wa pesa hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Momba Said Ilando alikiri kuwepo kwa kosa hilo na aliahidi kumchukulia hatua Mkandarasi huyo kwa matumizi mabovu ya fedha hizo, lakini pia kwa kushindwa kusimamia vizuri ujenzi huo licha ya kupata semina ya matumizi ya fedha mazuri kupitia akaunti inayohusisha jamii katika shughuli za ujenzi wa vituo hivyo yaani Forced akaunti.
Said ameendelea kusema kuwa kamati ya ujenzi ya kituo cha Afya cha Tunduma kwenda katika Halmashauri nyingine ambazo zinafanya vizuri katika ujenzi wa majengo hayo kwa gharama ndogo inayotokana na kutumia Forced akaunti.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dk. Kheri Kagya wakati anawasilisha taarifa yake amesema kuwa kiwango cha matumizi ya njia mbali mbali za uzazi wa mpango ni asilimia 45 ukilinganisha na asilimia 44.6 huku kiwango cha kitaifa kikiwa asilimia 27, huku changamoto ikiwa ni wajawazito kuchelewa kuanza kliniki mapema.
Dk.Kagya anasema kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kupitia huduma ya ushauri nasaha (VCT) ni asilimia 4 ambapo kitaifa kwa utafiti wa mwaka 2016/2017 (THIS) maambukizi ya UKIMWI ni asilimia 5.8 kwa Mkoa wa Songwe, aidha huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 40,988 wlipimwa VVU kati yao 1,616 asilimia 3 walikutwa na maambukizi ya VVU.
No comments:
Post a Comment