Wasimamizi uchaguzi Kinondoni wafundwa....soma habari kamili na matukio360..#share

Hussein Makame-NEC, Dar es Salaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi ili kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.
Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo.


Hayo yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo la jiji la Dar es Salaam.

Amesema wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni mchakato unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.

“Hivyo mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria...,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza” amesema Elisante.

Amewakumbusha wasimamizi hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekuwa ikisisitiza kwamba Sheria za Uchaguzi hazikuacha ombwe katika kueleza jinsi gani masuala ya Uchaguzi yanatakiwa yatatuliwe.

Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge akiwasilisha mada ya Maelekezo kwa wasimamizi hao, amewataka kutoruhusu matumizi ya utambulisho mwingine mbadala tofauti na ule ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeruhusu kutumika.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 61 (3) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, kimeipa mamlaka Tume kuidhinisha

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search