Prisons waipania Singida Utd...soma habari kamili na matukio 360...#share
Na mwandishi wetu,mbeya
TIMU ya Tanzania Prisons imepania kuchukua pointi tatu dhidi ya Singida United katika mchezo wao wa kufunga mzunguko wa kwanza wa ligi kuu utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Kikosi cha timu ya Prisons
Kikosi cha timu ya Prisons
Kocha Mkuu wa kikosi cha Wajela jela hao, Mohamed Abdallah amesema kuwa kwa wiki nzima timu imekuwa katika maandalizi mazito ya kuhakikisha inapata ushindi baada ya mchezo wa awali kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam.
Abdallah amesema baada ya matokeo hayo yasiyoridhisha yeye pamoja na wachezaji wamekubaliana kutorudia makosa yaliyoonekana kwenye mechi hiyo ya kwanza kufungwa nyumbani tangu kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara .
‘’Ni mchezo wa mpira hatuna budi kukubaliana na matokeo yaliyotupata ,hatujaridhishwa nayo lakini tutapambana ili kuhakikisha tunafuta makosa hayo katika mchezo wetu dhidi ya Singida hapo kesho kutwa(kesho),’’ame
sema Abdallah
sema Abdallah
Amesema pamoja na timu hiyo (Singida United) kuwa ngeni kwenye michuano ya Ligi msimu huu lakini wamekuja na upinzani wa hali ya juu ambao hauwezi kuwatisha wachezaji wake wakongwe na wenye vipaji .
Abdallah alibainisha kuwa jambo jema kwa mashabiki na wadau wa timu hiyo ni kwamba kikosi hakina majeruhi yeyote ,hivyo vijana wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Prisons inashika nafasi ya sita kimsimamo kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi , ikiwa imevuna pointi 21 kwa mechi 14 ilizocheza huku wapinzani wao Singida wakishika nafasi ya tano baada ya kuvuna pointi 24.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment