Polisi wapambana na wananchi DRC...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
POLISI katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaomtaka rais Joseph Kabila aondoke madarakani.
Polisi wa DRC wakipambana na wananchi
Watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wamekamatwa, wakiwemo waandishi habari.
Maafisa wamepiga marufuku maandamano hayo na huduma za intaneti zimefungwa.
Kanisa katoliki limewataka raia washirika katika maandamano ya amani baada ya misa ya Jumapili - wakibeba bibilia rosari na misalaba.
Maafisa wa usalama walikabiliana na maandamano hayo kwa kutumia nguvu katika miji tofuati nchini.
Katika mji mkuu Kinshasa, walinda amani wa Umoja wa mataifa wanaarifiwa kutawanywa kujaribu kuwatenganisha waandamanji na vikosi vya usalama nchini.
Kumeshuhudiwa maandamano mengi dhidi ya rais Kabila tangu muhula wake umalizike zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Congo inakabiliwa pia na mizozo kadhaa ya makundi ya kujihami, hususani katika maeneo ya mashariki na kati mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment