CCM: Hatuna muda wa kujadiliana na wapinzani...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Mwajuma Juma, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema  kwa sasa hawana muda tena wa kukutana na wapinzani kuzungumzia masuala ya uchaguzi na kazi iliyo mbele yao ni kupanga maendeleo.

Abdallah Juma Mabodi

Msimamo huo umetolewa na naibu katibu mkuu CCM Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa  katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui.

Amesema kwa sasa muda wa kujadili masuala ya siasa hapo kwa kuwa nafasi hiyo ilitolewa na wapinzani walidharau


“Hakuna mazungumzo tena kwa sasa tukutane 2020 katika uchaguzi,
washaona mambo yanakwenda vizuri wanaleta vidudu mtu”, alisema Mabodi.

“Walikuja wazungu hapa ofisini kwangu nikawaambia sisi suala la
uchaguzi limekwisha tunapanga maendeleao”, aliongeza naibu katibu mkuu huyo.

Amesema  wakati huo CCM iliwatumia wazee akiwamo Salmini, Karume na wengine wengi ili kuzungumzia sula hilo lakini walikataa.

“Tuliwahita  wazee wetu mkatuzungusha  sasa hivi wanataka nini
hatuna muda tena na Dk Shein huyo anapepea yupo  Uwarabuni kutafuta pesa”, alisema.

Samabamba na hilo aliwataka wanaCCM wa Shirikisho hilo kujitahidi kuwa mabalozi wazuri katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuingiza wanachama wapya na kuwashawishi kwenda kujiandikisha katika daftari la kupiga kura wale wote ambao tayari wameshafikia umri wa kupiga kura.

Amesema CCM pamoja na kuwa na wafanyakazi wengi ndani ya ofisi na
jumuia zao lakini bado nguvu za wanachama wa nje zinahitajika ili
kuweza kukiletea ushindi.

“Kama hatujawatumia wanaCCM waliopo nje ya ofisi zetu hatutofika
mbele, lazima tutumie jeshi la wanaCCM hawa kuwaelezea watu ili
kutengeneza mazingira mazuri ya ushindi," amesema.

Hata hivyo aliwataka wanashirikisho hilo kusoma katiba na kanuni za
chama na kujenga ushirikiano na viongozi wao katika kukijenga chama
na inapotokea matatizo wayatatuwe kulingana na katiba na kanuni
zinavyoelekeza.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search