Raila Odinga aapishwa kuwa rais wa wananchi Kenya....soma habari kamili na matukio360...#share
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameapishwa kuwa rais wa wananchi. Ameapishwa na mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang.
Wengi wajitokeza kushuhudia Odinga akila kiapo
Hata hivyo wakuu wa chama hicho akiwemo Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula hawakuwepo wakati wa kiapo hicho kilichochukuliwa katika eneo la Uhuru Park
Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga aliondoka huku maelfu waliokuwawakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.
Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika uwanja huo
Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya. Maelekezomengine mtayapata baadae."
Baada ya polisi kuondoka uwanja wa Uhuru Park, wafuasi wa upinzani walianza kuingia kwa wingi na kwa sasa maelfu wamo ndani.
No comments:
Post a Comment