Waziri mkuu aunguruma mkutano AU Ethiopia....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu,
Addis Ababa
WAZIRI
Mkuu Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha
katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Amesema hayo jana alipozungumza baada
ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis
Ababa, Ethiopia.
Katika
Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli, alisema
nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.
Waziri
Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua
kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Alisema
nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya
kuimarisha uzalishaji wa umeme.
“Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo
vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha
kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea
taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita.
Alisema
miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa inashughulikia masuala
ya usalama na amani katika Bara la Afrika.
Pia
Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi
za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo
kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa
Umoja wa Afrika.
Alisema
Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika nchi za
Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi jirani
pamoja na Jumuia zake.
No comments:
Post a Comment