Simba wamkaribisha kocha mpya kibabe...soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Simba imezidi kujichimbia
kileleni mwa msimamo wa ligi katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya
Tanzania Bara ‘VPL’ baada ya kuitandika bila huruma timu ya singida united kwa
magoli 4-0. Ushindi huo ni kama wamemkaribisha kocha wao mpya Mfaransa Pierre Lichantre kibabe
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya goli.
Ushindi huo katika mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam umeifanya Simba kufikisha pointi 29
huku ikimuacha kwa pointi mbili Azama iliyoko nafasi ya pili ikiwa na pointi
27, baada ya jana kulazimishwa sare 1-1 na Majimaji ya Songea.
Alikuwa Shiza Ramadhani Kichuya
alianza kuwanyanyua mashabiki wa Simba mnamo dakika ya 3 ya mchezo baada ya
faulo ya Mwinyi Kazimoto uzembe wa mabeki wa Singida ulimpa mwanya mfungaji wa
bao hilo.
Uzembe tena uliofanywa na mabeki wa
Singida wakidhani kuwa Simba wameotea dakika ya 23 benki kisiki aliyesajiliwa
toka Lipuli FC ,Asante Kwasi alifunga goli la pili huku likiwa la sita kwake na
la kwanza akiwa na jezi ya Simba.
Akitokea benchi Mshambuliaji hatari
mwenye kasi ya ajabu Emmanuel Okwi alifunga magoli mawili dakika ya 76 na 79 na
kufikisha jumla ya magoli 10 akifutiwa na mshambuliaji wa Mbao FC mwenye magoli
saba.
Kwa matokeo hayo pia Simba inamuacha
mtani wake wa jadi klabu ya Yanga kwa pointi 7 kwani kwa sasa bYanga imejikusanyia
pointi 22.
No comments:
Post a Comment