Majaliwa: Serikali kumaliza mgogoro wananchi na muwekezaji....soma habari kamili na matukio 360....#share
Na
Mwandishi Wetu, Mara
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza mgogoro ulipo kati
ya wananchi wa Kata ya Nyamongo na muwekezaji wa mgodi wa North Mara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi pamoja na mwekezaji wa mgodi huo
wanaishi na kuendesha shughuli zao za kimaendeleo kwa kufuata sheria za nchi.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 18, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Nyamongo, wilayani Tarime.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 18, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Nyamongo, wilayani Tarime.
Waziri
Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi na wawekezaji
wakigombana, inataka kumaliza mgogoro huo ili pande zote zifanye kazi zake kwa
amani.
Katika kuhakikisha mgogoro huo unakuwa historia Waziri Mkuu ameitisha kikao kitakachowakutanisha wawakilishi wa wananchi , viongozi wa mgodi na mbunge wa jimbo la Tarime John Heche.
Katika kuhakikisha mgogoro huo unakuwa historia Waziri Mkuu ameitisha kikao kitakachowakutanisha wawakilishi wa wananchi , viongozi wa mgodi na mbunge wa jimbo la Tarime John Heche.
Amesema
katika hicho kitakachofanyika Januari 28, 2018 Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini
Dodoma, ambapo aliwakikishia wananchi hao kwamba Serikali italinda maslahi yao.Awali,
Waziri Mkuu alitembelea kata ya Nyamwaga na kukagua kituo cha afya cha
Nyamwaga, ambapo amesema kinatosha kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya
wilaya.
Hivyo
amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Francis Mwanisi aanze mchakato wa
kupeleka vifaa katika kituo hicho ili wananchi wa Halmashauri ya Tarime waanze
kutibiwa.
Waziri
Mkuu amesema Rais Dkt. John Magufuli ameongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na
kufikia sh. bilioni 269 ili kuhakikisha hakuna mgonjwa anayekwenda hospitali na
kukosa dawa.
Amesema
mbali na kuongeza bajeti katika ununuzi wa dawa, pia ameziagiza halmashauri
zote kuhakikisha suala la utoaji wa vitambulisho kwa wazee ili watibiwe bure
linatekelezwa
No comments:
Post a Comment