Tecno kuzindua simu mpya...soma habari kamili na matukio360...#share

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Tecno inatarajia kuzindua toleo jipya la simu.

Uzinduzi huo ni utaratibu kwa kila mwaka, kampuni ya TECNO kuzindua simu mpya na hua ni muendelezo wa matoleo yaliopita.


Kwa mwaka huu TECNO wanaachilia simu ikiwa ni muendelezo wa simu aina ya CAMON. Camon imekua moja wapo ya simu janja (smartphone) pendwa sana kwa wadau kwa mwaka 2017!


Wanatarajia kuitoa simu hiyo ndani ya mwezi(Januari – Machi) 2018 na itakuwa ni simu ya kipekee kwa kuwa ina vigezo maalumu kulinganisha na simu zingine zilizopita kabla


Kadri miaka inavyosogea na kuendelea teknolojia ya simu, miundo ya simu, vigezo, mahitaji na matumizi ya simu hubadilika na kuongezeka, hivyo kama kampuni imekua ni jambo muhimu kuweza kutoa simu zinazokidhi mahitaji ya wadau na watumiaji wa bidhaa zake hivyo kutoa toleo jipya kabisa!
Je, ni simu gani na itakua na vigezo/muundo gani?

Fuatilia kurasa za TECNO katika mitandao ya kijamii na tovuti yao kujua zaidi!

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search